Mhubiri 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mhubiri 10 (Swahili) Ecclesiastes 10 (English)

Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima. Mhubiri 10:1

Dead flies cause the oil of the perfumer to send forth an evil odor; so does a little folly outweigh wisdom and honor.

Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto. Mhubiri 10:2

A wise man's heart is at his right hand, but a fool's heart at his left.

Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu. Mhubiri 10:3

Yes also, when the fool walks by the way, his understanding fails him, and he says to everyone that he is a fool.

Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa. Mhubiri 10:4

If the spirit of the ruler rises up against you, don't leave your place; for gentleness lays great offenses to rest.

Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; Mhubiri 10:5

There is an evil which I have seen under the sun, the sort of error which proceeds from the ruler.

ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini. Mhubiri 10:6

Folly is set in great dignity, and the rich sit in a low place.

Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa. Mhubiri 10:7

I have seen servants on horses, and princes walking like servants on the earth.

Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma. Mhubiri 10:8

He who digs a pit may fall into it; and whoever breaks through a wall may be bitten by a snake.

Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo. Mhubiri 10:9

Whoever carves out stones may be injured by them. Whoever splits wood may be endangered thereby.

Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa. Mhubiri 10:10

If the axe is blunt, and one doesn't sharpen the edge, then he must use more strength; but skill brings success.

Nyoka akiuma asijatumbuizwa, Basi hakuna faida ya mtumbuizi. Mhubiri 10:11

If the snake bites before it is charmed, then is there no profit for the charmer's tongue.

Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake. Mhubiri 10:12

The words of a wise man's mouth are gracious; but a fool is swallowed by his own lips.

Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari. Mhubiri 10:13

The beginning of the words of his mouth is foolishness; and the end of his talk is mischievous madness.

Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza? Mhubiri 10:14

A fool also multiplies words. Man doesn't know what will be; and that which will be after him, who can tell him?

Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, Maana hajui hata njia ya kuuendea mji. Mhubiri 10:15

The labor of fools wearies every one of them; for he doesn't know how to go to the city.

Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi! Mhubiri 10:16

Woe to you, land, when your king is a child, And your princes eat in the morning!

Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi. Mhubiri 10:17

Happy are you, land, when your king is the son of nobles, And your princes eat in due season, For strength, and not for drunkenness!

Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja. Mhubiri 10:18

By slothfulness the roof sinks in; And through idleness of the hands the house leaks.

Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote. Mhubiri 10:19

A feast is made for laughter, And wine makes the life glad; And money is the answer for all things.

Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako; Wala usiwalaani wakwasi chumbani mwako; Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, Na mwenye mabawa ataitoa habari. Mhubiri 10:20

Don't curse the king, no, not in your thoughts; And don't curse the rich in your bedchamber: For a bird of the sky may carry your voice, And that which has wings may tell the matter.